Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika tulimletea Mūsā Taurati kama tulivyokuletea wewe, ewe Mtume, Qur’ani. Basi usiwe na shaka ya kukutana na Mūsā usiku wa Isrā’ (safari ya kwenda Bayt al- Maqdis) na Mi’rāj (safari ya kwenda mbinguni), na tukaifanya Taurati ni uongofu kwa Wana wa Isrāīl, Unawalingania kwenye haki na kwenye njia iliyonyoka.