Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ni Wake Yeye, kutakasika ni Kwake, ufalme wa mbinguni na ardhini, na mkononi Mwake kuna funguo za rehema na riziki, Anamkunjulia riziki Yake Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na Anambania Anayemtaka. Hakika Yeye , Aliyetukuka na kuwa juu, ni Mjuzi wa kila kitu, Hakifichamani Kwake Yeye chochote katika mambo ya viumbe Vyake.