Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Anampa, Anayetakasika na kutukuka, Anayemtaka miongoni mwa watu wanaume na wanawake. Na Anamfanya Anayemtaka kuwa tasa asiyezaa. Hakika Yeye ni Mjuzi sana wa Anachoumba, ni Muweza sana kuumba Anachotaka, hakuna chochote kinachomshinda Akitaka kukiumba.