Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni mardufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukra, Mpole. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Iwapo mtatoa mali yenu katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Yeye na kwa moyo mzuri, Atawaongezea Mwenyezi Mungu thawabu za ambacho mmekitoa na Atawasamehe madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kurudisha shukrani kwa watoaji kwa kuwapa malipo mema ya kile walichokitoa, ni Mpole kwa kutoharakisha mateso kwa wanaomuasi.