Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walidai wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu kwa ubatilifu kwamba wao hawatatolewa kwenye makaburi yao baada ya kufa. Waambie, ewe Mtume, «Ndio. Naapa kwa Mola wangu! Mtatolewa makaburini mwenu mkiwa hai, kisha mtapewa habari ya yale mliyoyafanya duniani. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali na rahisi.