Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: At-Talaq 65:1

65:1
يا ايها النبي اذا طلقتم النساء فطلقوهن لعدتهن واحصوا العدة واتقوا الله ربكم لا تخرجوهن من بيوتهن ولا يخرجن الا ان ياتين بفاحشة مبينة وتلك حدود الله ومن يتعد حدود الله فقد ظلم نفسه لا تدري لعل الله يحدث بعد ذالك امرا ١
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا۟ ٱلْعِدَّةَ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّآ أَن يَأْتِينَ بِفَـٰحِشَةٍۢ مُّبَيِّنَةٍۢ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُۥ ۚ لَا تَدْرِى لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًۭا ١
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلنَّبِيُّ
إِذَا
طَلَّقۡتُمُ
ٱلنِّسَآءَ
فَطَلِّقُوهُنَّ
لِعِدَّتِهِنَّ
وَأَحۡصُواْ
ٱلۡعِدَّةَۖ
وَٱتَّقُواْ
ٱللَّهَ
رَبَّكُمۡۖ
لَا
تُخۡرِجُوهُنَّ
مِنۢ
بُيُوتِهِنَّ
وَلَا
يَخۡرُجۡنَ
إِلَّآ
أَن
يَأۡتِينَ
بِفَٰحِشَةٖ
مُّبَيِّنَةٖۚ
وَتِلۡكَ
حُدُودُ
ٱللَّهِۚ
وَمَن
يَتَعَدَّ
حُدُودَ
ٱللَّهِ
فَقَدۡ
ظَلَمَ
نَفۡسَهُۥۚ
لَا
تَدۡرِي
لَعَلَّ
ٱللَّهَ
يُحۡدِثُ
بَعۡدَ
ذَٰلِكَ
أَمۡرٗا
١
Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ewe Mtume! Pindi mnapotaka, wewe na Waumini, kuwapa talaka wake zenu, basi wapeni talaka wakiwa kwenye hali ya kukabili kipindi cha wao kukaa eda- yaani kwenye hali ya usafi ambao hakukupatikana kuingiliwa, au katika hali ya mimba iliyo wazi- na mshike hesabu ya eda, mpate kujua muda wa kuwarejea iwapo mtataka kuwarejea, na muogopeni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Wala msiwatoe wanawake waliopewa talaka kwenye majumba wanayokaa mpaka eda lao limalizike, nalo ni hedhi tatu kwa asiyekuwa mdogo (asiyeingia damuni) na si kwa aliyekata tamaa ya kuingia damuni (kwa uzee) wala mwenye mimba. Na haifai kwa wanawake hao kutoka majumbani mwao wao wenyewe isipokuwa watakapofanya kitendo kiovu cha waziwazi kama vile uzinifu. Na hizo ndizo hukumu za Mwenyezi Mungu alizozipitisha kwa waja Wake. Na Mwenye kuzikiuka hukumu za Mwenyezi Mungu, basi huyo amejidhulimu nafsi yake na ameipeleka mahali pa maangamivu. Hujui, ewe mtoaji talaka, kwamba Mwenyezi Mungu huenda, baada ya talaka hiyo, Akaleta jambo usilolitazamia ukaja ukamrudia.