Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: At-Talaq 65:2

65:2
فاذا بلغن اجلهن فامسكوهن بمعروف او فارقوهن بمعروف واشهدوا ذوي عدل منكم واقيموا الشهادة لله ذالكم يوعظ به من كان يومن بالله واليوم الاخر ومن يتق الله يجعل له مخرجا ٢
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍۢ وَأَشْهِدُوا۟ ذَوَىْ عَدْلٍۢ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا۟ ٱلشَّهَـٰدَةَ لِلَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مَخْرَجًۭا ٢
فَإِذَا
بَلَغۡنَ
أَجَلَهُنَّ
فَأَمۡسِكُوهُنَّ
بِمَعۡرُوفٍ
أَوۡ
فَارِقُوهُنَّ
بِمَعۡرُوفٖ
وَأَشۡهِدُواْ
ذَوَيۡ
عَدۡلٖ
مِّنكُمۡ
وَأَقِيمُواْ
ٱلشَّهَٰدَةَ
لِلَّهِۚ
ذَٰلِكُمۡ
يُوعَظُ
بِهِۦ
مَن
كَانَ
يُؤۡمِنُ
بِٱللَّهِ
وَٱلۡيَوۡمِ
ٱلۡأٓخِرِۚ
وَمَن
يَتَّقِ
ٱللَّهَ
يَجۡعَل
لَّهُۥ
مَخۡرَجٗا
٢
Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na pindi kipindi cha eda la wanawake waliopewa talaka kinapokaribia kumalizika, basi warudieni na mtangamane nao kwa wema pamoja na kuwapatia matumizi, au waacheni pamoja na kuwatekelezea haki zao bila kuwafanyia mambo ya kuwadhuru. Na wekeni mashahidi mnaporejeana na mnapoachana, wanaume wawili waadilifu miongoni mwenu. Na tekelezeni, enyi mashahidi, ushahidi wenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na sio kwa kitu kingine. Hilo ambalo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha kwalo yuwawaidhiwa nalo yule anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na yoyote atakayemuogopa Mwenyezi Mungu akayafuata kivitendo yale ambayo Amemuamrisha nayo na akayaepuka yale ambayo Amemkataza nayo, Atamtolea njia ya kutoka kwenye kila dhiki