Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hayo yailotajwa kuhusiana na mambo ya talaka na eda ni amri ya Mwenyezi Mungu Aliyoiteremsha kwenu, enyi watu, ili muitumie. Na yoyote mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu akawa anamcha kwa kuyaepuka yale ya kumuasi na kuzitekeleza faradhi Zake, basi Atamfutia madhambi yake, Atamuongezea kwa wingi malipo yake huko Akhera na amuingize Peponi.