Hakika Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi; huhuisha na hufisha. Nanyi hamna Mlinzi wala Msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Mwenyezi Mungu ni mmiliki wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, Hana mshirika katika uumbaji, uendeshaji, ustahiki wa kuabudiwa na uwekaji sheria. Anampa uhai Anayemtaka na anamfisha Anayemtaka. Na hakuna yoyote, isipokuwa Mwenyezi Mungu, wa kuyasimamia mambo yenu wala wakuwapa ushindi juu ya adui wenu.