Wale walio amini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufuzu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakaiacha Nyumba ya ukafiri wakielekea kwenye Nyumba ya Uislamu na wakatoa mali zao na nafsi zao katika jihadi ili kulikuza neno la Mwenyezi Mungu. Hawa wana daraja kubwa mno kwa Mwenyezi Mungu, na wao ndio wenye kufaulu kuzipata radhi Zake.