Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: At-Tawba 9:44

9:44
لا يستاذنك الذين يومنون بالله واليوم الاخر ان يجاهدوا باموالهم وانفسهم والله عليم بالمتقين ٤٤
لَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أَن يُجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُتَّقِينَ ٤٤
لَا
يَسۡتَـٔۡذِنُكَ
ٱلَّذِينَ
يُؤۡمِنُونَ
بِٱللَّهِ
وَٱلۡيَوۡمِ
ٱلۡأٓخِرِ
أَن
يُجَٰهِدُواْ
بِأَمۡوَٰلِهِمۡ
وَأَنفُسِهِمۡۗ
وَٱللَّهُ
عَلِيمُۢ
بِٱلۡمُتَّقِينَ
٤٤
Hawatakuomba ruhusa wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wasende kupigana Jihadi kwa mali yao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua wachamngu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Si katika misimamo ya wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Siku ya Mwisho kukutaka ruhusa, ewe Nubii, ya kusalia nyuma kwa kutoshiriki kwenye jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi na mali. Hiyo ni misimamo ya wanafiki tu. Na Mwenyezi Mungu Anamjua Anayemuogopa Yeye na kumcha kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kujitenga na Makatazo Yake.