Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: At-Tawba 9:48

9:48
لقد ابتغوا الفتنة من قبل وقلبوا لك الامور حتى جاء الحق وظهر امر الله وهم كارهون ٤٨
لَقَدِ ٱبْتَغَوُا۟ ٱلْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا۟ لَكَ ٱلْأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَهُمْ كَـٰرِهُونَ ٤٨
لَقَدِ
ٱبۡتَغَوُاْ
ٱلۡفِتۡنَةَ
مِن
قَبۡلُ
وَقَلَّبُواْ
لَكَ
ٱلۡأُمُورَ
حَتَّىٰ
جَآءَ
ٱلۡحَقُّ
وَظَهَرَ
أَمۡرُ
ٱللَّهِ
وَهُمۡ
كَٰرِهُونَ
٤٨
Tangu zamani walitaka kukutilieni fitna, na wakakupindulia mambo juu chini, mpaka ikaja Haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu, na wao wamechukia. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walipendelea wanafiki kuwafitini Waumini na Dini yao na kuwazuia wasiiifuate njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya vita vya Tabūk, na mambo yao yakafunuka wakajulikana. Na walikuchafulia mambo, ewe Nabii, katika kuyavunja uliyokuja nayo, kama walivyofanya siku ya vita vya Uḥud na siku ya vita vya Khandaq. Na walikufanyia vitimbi mpaka usaidizi ukaja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Akawatia nguvu askari Wake na Akaipa ushindi dini Yake, pamoja na kuwa wao wanaichukia.