Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
9:47
لو خرجوا فيكم ما زادوكم الا خبالا ولاوضعوا خلالكم يبغونكم الفتنة وفيكم سماعون لهم والله عليم بالظالمين ٤٧
لَوْ خَرَجُوا۟ فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًۭا وَلَأَوْضَعُوا۟ خِلَـٰلَكُمْ يَبْغُونَكُمُ ٱلْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّـٰعُونَ لَهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ ٤٧
لَوۡ
خَرَجُواْ
فِيكُم
مَّا
زَادُوكُمۡ
إِلَّا
خَبَالٗا
وَلَأَوۡضَعُواْ
خِلَٰلَكُمۡ
يَبۡغُونَكُمُ
ٱلۡفِتۡنَةَ
وَفِيكُمۡ
سَمَّٰعُونَ
لَهُمۡۗ
وَٱللَّهُ
عَلِيمُۢ
بِٱلظَّٰلِمِينَ
٤٧
Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Lau wanafiki wangalitoka pamoja na nyinyi, enyi Waumini, kwenye jihadi, wangalieneza mgongano katika safu zenu, ubaya na uharibifu, na wanagalikimbilia kueneza fitina na chuki baina yenu, kwa lengo la kutaka kuwafitini kwa kuwazorotesha msipigane jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na katika nyinyi, enyi Waumini, kuna wapelelezi wa makafiri, wanazisikia habari zenu na wanazipeleka kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno wa wanafiki walio madhalimu na Atawalipa kwa hilo.