Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hawa washirikina waliwafanya Malaika ambao ni waja wa Mwenyezi Mungu kuwa ni wanawake. Je, wao walihudhuria wakati Mwenyezi Mungu Alipowaumba mpaka waamue kuwa wao ni wanawake? Ushahidi wao utasajiliwa, na wataulizwa kuhusu hilo kesho Akhera.