Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
043

Az-Zukhruf 43:47 فلما جاءهم باياتنا اذا هم منها يضحكون ٤٧

43:47
فَلَمَّا
جَآءَهُم
بِـَٔايَٰتِنَآ
إِذَا
هُم
مِّنۡهَا
يَضۡحَكُونَ
٤٧
Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Na alipowajia na dalili zilizo wazi zenye kuonyesha ukweli wake katika ulinganizi wake, hapo Fir’awn na viongozi wa utawala wake wakawa wanazicheka zile hoja na mazingatio alivyokuja navyo Mūsā.
Na alipowajia na dalili zilizo wazi zenye kuonyesha ukweli wake katika ulinganizi wake, hapo Fir’awn na viongozi wa utawala wake wakawa wanazicheka zi…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 43, Ukurasa 492, Juzuu 25

46. Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote! 47. Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka. 48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. 49. Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. 50. Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi. 51. Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni? 52. Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? 53. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama? 54. Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. 55. Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote! 56. Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote!

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia