Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Fir’awn na viongozi wa utawala wake wakasema kumwambia Mūsā, ”Ewe mjuzi! (Na mchawi alikuwa kwao ni mtu mkubwa wanayemheshimu, na haukuwa uchawi ni sifa ya mtu kutukanika), ’Tuombee Mola wako, kwa ile ahadi Aliyokuahidi na yale matukufu Aliyokutunukia wewe mahsusi, Atuepushie adhabu, kwani tukiepushiwa adhabu, kwa hakika sisi ni wenye kuongoka na kuayaamini yale uliotujia nayo.