Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watazungushiwa, hawa waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, chakula ndani ya vyombo vya dhahabu na vinywaji ndani ya gilasi za dhahabu. Na humo watakuwa na kila ambacho nafsi zao zinakitamani na macho yao yanapendezwa nacho, na wao humo watakaa milele.