Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina wa watu wako, ”Ni nani aliyewaumba?” watasema, «Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyetuumba.” Basi vipi wao wanageuka na wanapotoka kwa kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na kumshirikisha na asiyekuwa Yeye?