Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Az-Zumar 39:10

39:10
قل يا عباد الذين امنوا اتقوا ربكم للذين احسنوا في هاذه الدنيا حسنة وارض الله واسعة انما يوفى الصابرون اجرهم بغير حساب ١٠
قُلْ يَـٰعِبَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةٌۭ ۗ وَأَرْضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى ٱلصَّـٰبِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍۢ ١٠
قُلۡ
يَٰعِبَادِ
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
ٱتَّقُواْ
رَبَّكُمۡۚ
لِلَّذِينَ
أَحۡسَنُواْ
فِي
هَٰذِهِ
ٱلدُّنۡيَا
حَسَنَةٞۗ
وَأَرۡضُ
ٱللَّهِ
وَٰسِعَةٌۗ
إِنَّمَا
يُوَفَّى
ٱلصَّٰبِرُونَ
أَجۡرَهُم
بِغَيۡرِ
حِسَابٖ
١٠
Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Nabii, kuwaambia waja wangu wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, «Mcheni Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kujiepusha na matendo ya kumuasi.» Na wale waliofanya wema katika dunia hii kwa kumuabudu Mola wao na kumtii watapata wema huko Akhera, nao ni pepo, na wema huko duniani, ambao ni afya, riziki, ushindi na vinginevyo. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu, basi hamieni humo muende pale ambapo mtamuabudu Mola wenu na mtamakinika kusimamisha Dini yenu. Hakika Mwenyezi Mungu Atawapa wenye kuvumilia malipo yao mema huko Akhera bila mpaka wala hesabu wala kipimo. Huku ni kuyafanya makubwa malipo ya wenye kusubiri na thawabu zao.