Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Az-Zumar 39:15

39:15
فاعبدوا ما شيتم من دونه قل ان الخاسرين الذين خسروا انفسهم واهليهم يوم القيامة الا ذالك هو الخسران المبين ١٥
فَٱعْبُدُوا۟ مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِۦ ۗ قُلْ إِنَّ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْخُسْرَانُ ٱلْمُبِينُ ١٥
فَٱعۡبُدُواْ
مَا
شِئۡتُم
مِّن
دُونِهِۦۗ
قُلۡ
إِنَّ
ٱلۡخَٰسِرِينَ
ٱلَّذِينَ
خَسِرُوٓاْ
أَنفُسَهُمۡ
وَأَهۡلِيهِمۡ
يَوۡمَ
ٱلۡقِيَٰمَةِۗ
أَلَا
ذَٰلِكَ
هُوَ
ٱلۡخُسۡرَانُ
ٱلۡمُبِينُ
١٥
Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika walio khasirika ni wale walio jikhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo khasara iliyo dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi nyinyi, enyi washirikina, abuduni mnachotaka badala ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa mizimu na masanamu na visiokuwa hivyo katika viumbe Vyake, kwani hilo halinidhuru mimi chochote.» Na hili ni onyo na tahadharisho kwa anayemuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na akamshirikisha mwingine pamoja na Yeye. Sema, ewe Mtume, «Hakika wale wenye hasara kikweli ni wale watakaohasirika nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama.» Na hiyo ni kwa sababu ya kuwapoteza duniani na kuwapotosha na njia ya Imani. Jua utanabahi kwamba hawa washirikina kupata hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama ndiko kupata hasara kuliofunuka waziwazi.