Na aliye ileta Kweli na akaithibitisha - hao ndio wachamngu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na yule aliyekuja na ukweli wa maneno na vitendo, miongoni mwa Manabii na wafuasi wao, na akaukubali kiimani na kivitendo, hao ndio waliokusanya sifa za uchamungu, akiwa mbele yao yule aliye mwisho wa Manabii na Mitume, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wale wenye kumuamini, wanaoifuata Sheria yake kivitendo miongoni mwa Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie, kisha wale wenye kuja baada yao mpaka Siku ya Malipo.