Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sisi tumekutumiliza kwa haki, nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Sheria za Dini, hali ya kuwapa bishara ya Pepo wale wenye kukuamini na wakaufuata uongofu wako kivitendo, na hali ya kuwaonya Moto wale waliokukanusha na wakakuasi. Na hakuna taifa lolote la watu isipokuwa limejiwa na muonyaji wa kuwaonya mwisho mbaya wa ukafiri wao na upotevu wao.