Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Fatir 35:32

35:32
ثم اورثنا الكتاب الذين اصطفينا من عبادنا فمنهم ظالم لنفسه ومنهم مقتصد ومنهم سابق بالخيرات باذن الله ذالك هو الفضل الكبير ٣٢
ثُمَّ أَوْرَثْنَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌۭ لِّنَفْسِهِۦ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌۭ وَمِنْهُمْ سَابِقٌۢ بِٱلْخَيْرَٰتِ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْكَبِيرُ ٣٢
ثُمَّ
أَوۡرَثۡنَا
ٱلۡكِتَٰبَ
ٱلَّذِينَ
ٱصۡطَفَيۡنَا
مِنۡ
عِبَادِنَاۖ
فَمِنۡهُمۡ
ظَالِمٞ
لِّنَفۡسِهِۦ
وَمِنۡهُم
مُّقۡتَصِدٞ
وَمِنۡهُمۡ
سَابِقُۢ
بِٱلۡخَيۡرَٰتِ
بِإِذۡنِ
ٱللَّهِۚ
ذَٰلِكَ
هُوَ
ٱلۡفَضۡلُ
ٱلۡكَبِيرُ
٣٢
Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliye tangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kisha tukawapa Qur’ani, baada ya ummah waliopita kuangamia, wale tuliowachagua miongoni mwa umati wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie: kati yao kuna aliyeidhulumu nafsi yake kwa kufanya baadhi ya maasia, na kati yao kuna aliyekuwa wastani, naye ni yule mwenye kutekeleza yaliyo wajibu na kuepuka yaliyoharamishwa, na katika wao kuna mwenye kutangulia kufanya mambo ya kheri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, yaani mwenye kukimbilia na kujitahidi kufanya amali njema, za faradhi na za ziada. Na kupewa Kitabu huko na kuchaguliwa ummah huu ndio nyongeza kubwa.