Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Fatir 35:38

35:38
ان الله عالم غيب السماوات والارض انه عليم بذات الصدور ٣٨
إِنَّ ٱللَّهَ عَـٰلِمُ غَيْبِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ٣٨
إِنَّ
ٱللَّهَ
عَٰلِمُ
غَيۡبِ
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَٱلۡأَرۡضِۚ
إِنَّهُۥ
عَلِيمُۢ
بِذَاتِ
ٱلصُّدُورِ
٣٨
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anakiona kila kisichoonekana mbinguni na ardhini, na kwa hakika Yeye ni Mjuzi mno wa vilivyofichamana nyoyoni. Basi muogopeni Asiwaone mkiwa mko katika hali ya kudhamiria shaka au ushirikina katika kumpwekeshaYeye au juu ya unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani ziwashukie, au muende kinyume na amri Yake katika mambo madogo ya hayo.