Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Fatir 35:44

35:44
اولم يسيروا في الارض فينظروا كيف كان عاقبة الذين من قبلهم وكانوا اشد منهم قوة وما كان الله ليعجزه من شيء في السماوات ولا في الارض انه كان عليما قديرا ٤٤
أَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةًۭ ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعْجِزَهُۥ مِن شَىْءٍۢ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمًۭا قَدِيرًۭا ٤٤
أَوَلَمۡ
يَسِيرُواْ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
فَيَنظُرُواْ
كَيۡفَ
كَانَ
عَٰقِبَةُ
ٱلَّذِينَ
مِن
قَبۡلِهِمۡ
وَكَانُوٓاْ
أَشَدَّ
مِنۡهُمۡ
قُوَّةٗۚ
وَمَا
كَانَ
ٱللَّهُ
لِيُعۡجِزَهُۥ
مِن
شَيۡءٖ
فِي
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَلَا
فِي
ٱلۡأَرۡضِۚ
إِنَّهُۥ
كَانَ
عَلِيمٗا
قَدِيرٗا
٤٤
Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, hawatembei makafiri wa Makkah kwenye ardhi, wakaona ulikuwa vipi mwisho wa wale waliokuwa kabla yao, kama vile 'Ād, Thamūd na mfano wao, na yale yaliyowapata ya maangamivu na yaliyowapata majumba yao ya uharibifu walipowakanusha Mitume, na makafiri hao walikuwa ni wakali zaidi na ni wenye nguvu zaidi kuliko makafiri wa Makkah? Na hakuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kuna kitu chochote mbinguni wala ardhini chenye kumlemea na kumpita. Hakika Yeye ni Mjuzi sana wa matendo yao ni Mwenye uweza wa kuwaangamiza.