Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Fatir 35:8

35:8
افمن زين له سوء عمله فراه حسنا فان الله يضل من يشاء ويهدي من يشاء فلا تذهب نفسك عليهم حسرات ان الله عليم بما يصنعون ٨
أَفَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ فَرَءَاهُ حَسَنًۭا ۖ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ ۖ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَٰتٍ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا يَصْنَعُونَ ٨
أَفَمَن
زُيِّنَ
لَهُۥ
سُوٓءُ
عَمَلِهِۦ
فَرَءَاهُ
حَسَنٗاۖ
فَإِنَّ
ٱللَّهَ
يُضِلُّ
مَن
يَشَآءُ
وَيَهۡدِي
مَن
يَشَآءُۖ
فَلَا
تَذۡهَبۡ
نَفۡسُكَ
عَلَيۡهِمۡ
حَسَرَٰتٍۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
عَلِيمُۢ
بِمَا
يَصۡنَعُونَ
٨
Je! Yule aliye pambiwa a'mali zake mbaya na akaziona ni njema - basi hakika Mwenyezi Mungu humwacha akapotea amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anajua wanayo yafanya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, yule ambaye Shetani anampambia matendo yake maovu ya kumuasi Mwenyezi Mungu, kukufuru na kuwaabudu wasiyekuwa Yeye miongoni mwa waungu na masanamu, akayaona ni mazuri yenye kupendeza, (Je, yeye) ni kama yule ambaye Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amemuongoza akaliona zuri kuwa ni zuri na ovu kuwa ni ovu? Hakika Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayemtaka na Anamuongoza Anayemtaka. Basi usijiangamize kwa kuwa na huzuni juu ya ukanushaji wa hawa waliopotea. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua maovu yao na Atawalipa kwa hayo malipo mabaya kabisa.