Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ha-Mym-Sajdah 41:25

41:25
۞ وقيضنا لهم قرناء فزينوا لهم ما بين ايديهم وما خلفهم وحق عليهم القول في امم قد خلت من قبلهم من الجن والانس انهم كانوا خاسرين ٢٥
۞ وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَآءَ فَزَيَّنُوا۟ لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ فِىٓ أُمَمٍۢ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ خَـٰسِرِينَ ٢٥
۞ وَقَيَّضۡنَا
لَهُمۡ
قُرَنَآءَ
فَزَيَّنُواْ
لَهُم
مَّا
بَيۡنَ
أَيۡدِيهِمۡ
وَمَا
خَلۡفَهُمۡ
وَحَقَّ
عَلَيۡهِمُ
ٱلۡقَوۡلُ
فِيٓ
أُمَمٖ
قَدۡ
خَلَتۡ
مِن
قَبۡلِهِم
مِّنَ
ٱلۡجِنِّ
وَٱلۡإِنسِۖ
إِنَّهُمۡ
كَانُواْ
خَٰسِرِينَ
٢٥
Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyo pita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kukhasirika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tuliwawekea hawa madhalimu wenye kukanusha marafiki wabaya miongoni mwa Mashetani wa kibinadamu na wa kijini, wakawapambia matendo yao machafu duniani, wakawaita kwenye ladha zake na matamanio yake ya haramu, na wakawapambia wao yaliyo nyuma yao katika mambo ya Akhera wakawasahaulisha wasiikumbuke, na wakawalingania wakatae Marejeo (ya Kiyama). Na kwa hjvyo walistahili kuingia Motoni wawe miongoni mwa wale makafiri wa ummah waliopita wa kijini na wa kibinadamu. Wao walikuwa wamepata hasara ya matendo yao duniani na hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama.