Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hawaafikiwi kwenye mambo haya yanayosifika vyema isipokuwa wale wanaojisubirisha juu ya mambo ambayo nafsi zao zinayachukia na wakajilazimisha kwa yale Anayoyapenda Mwenyezi Mungu. Na haafikiwi hayo isipokuwa mwenye fungu kubwa la hali njema ya duniani na Akhera.