Na Shet'ani akikuchochea kwa uchochezi wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Shetani anapotia ndani ya nafsi yako ushawishi wa mawazo ya kukufanya umlipe mbaya kwa ubaya, basi omba himaya ya Mwenyezi Mungu na ushikamane na Yeye. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia sana maombi yako ya kujilinda Kwake, ni Mwenye kuyajua sana mambo ya viumbe Vyake vyote.