Na tukimneemesha mwanaadamu hugeuka na kujitenga upande, na inapo mgusa shari, huwa na madua marefu marefu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tunapomneemesha binadamu kwa afya na riziki au vingineyo, hugeuka na kufanya kiburi kwa kukataa kuifuata haki. Na akipatikana na shida huwa akileta dua ndefu akimuomba Mwenyezi Mungu Amuondolee shida yake; huwa akimjua Mola wake wakati wa shida na hamjui wakati wa neema.