Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyo mpata husema: Taabu zimekwisha niondokea. Hakika yeye hujitapa na kutafakhari. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na lau tutamnyoshea mwanadamu dunia yake na tukamkunjulia riziki yake baada ya dhiki za maisha, atasema hapo, «Nimeondokewa na dhiki na shida.» Hakika yeye ni mwenye kujigamba kwa hizo neema, ni mwenye kuendelea sana katika kujifahiri na kujitukuza kwa watu.