Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu kiziwi, na mwenye kuona na anasikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamfikiri? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mfano wa makundi mawili, ya ukafiri na Imani, ni mfano wa kipofu asiyeona na kiziwi asiyesikia na yule anayeona na kusikia: kundi la ukafiri haliioni haki likapata kuifuata wala halimsikii mlinganizi wa Mwenyezi Mungu likapata kuongoka kwa sababu yake. Ama kundi la Imani limishaziona hoja za Mwenyezi Mungu na limemsikia mlinganizi wa Mwenyezi Mungu na limemuitikia. Je, yanafanana makundi mawili haya? Kwani hamzingatii na mkafikiri?