Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni wazushi tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tuliwamtumia watu wa kabila la 'Ād ndugu yao Hūd. Alisema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Basi mtakasieni Yeye ibada. Kwani nyinyi hamkuwa, katika kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni warongo.