Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Hud 11:57

11:57
فان تولوا فقد ابلغتكم ما ارسلت به اليكم ويستخلف ربي قوما غيركم ولا تضرونه شييا ان ربي على كل شيء حفيظ ٥٧
فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّآ أُرْسِلْتُ بِهِۦٓ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّى قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ رَبِّى عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَفِيظٌۭ ٥٧
فَإِن
تَوَلَّوۡاْ
فَقَدۡ
أَبۡلَغۡتُكُم
مَّآ
أُرۡسِلۡتُ
بِهِۦٓ
إِلَيۡكُمۡۚ
وَيَسۡتَخۡلِفُ
رَبِّي
قَوۡمًا
غَيۡرَكُمۡ
وَلَا
تَضُرُّونَهُۥ
شَيۡـًٔاۚ
إِنَّ
رَبِّي
عَلَىٰ
كُلِّ
شَيۡءٍ
حَفِيظٞ
٥٧
Na ikiwa watarudi nyuma, basi mimi nimekwisha kufikishieni niliyo tumwa kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Mkiyapa mgongo yale ninayowalingania kwayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada, basi nimeshaufikisha ujumbe wa Mola wangu kwneu na hoja ishasimama kwenu nyinyi, na Mwenyezi Mungu atawaangamiza kwa kuwa hamkumuamini, na Atawaleta watu wengine ambao watashika nafasi zenu katika majumba yenu na mali yenu, na ambao watamtakasia Mwenyezi Mungu ibada. Na nyinyi hamtamdhuru Yeye kitu chochote. Hakika Mola wangu amekidhibiti kila kitu na kukihifadhi; Yeye Ndiye Mwenye kunitunza msinifanyie ubaya.