NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Amechukua dhamana kuviruzuku vyote vinavyotambaa kwenye uso wa ardhi, kwa hisani Yake, na Anajua mahala pa kutulia kwake katika uhai wake na baada ya kufa kwake, na Anajua mahala ambapo vitakufa. Yote hayo yameandikwa kwenye Kitabu kilichoko kwa Mwenyezi Mungu chenye kueleza yote hayo.