Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi! Hakika kina A'adi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina A'adi, kaumu ya Huud. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wakafuatiwa, katika ulimwengu huu, na laana ya Mwenyezi Mungu, na wakafuatwa na hasira Zake Siku ya Kiyama. Jueni mtanabahi kwamba 'Ād walimkanusha Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake. Jueni mtanabahi kwamba umbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na maangamivu yatawashukia 'Ād, watu wa Hūd, kwa sababu ya ushirikina wao na kukanusha kwao neema ya Mola wao.