Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut'. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Alipoona Ibrāhīm kuwa mikono yao haifikikishwi kwenye yule mwanang>ombe aliyewaletea na kuwa wao hawamli, alikataa hilo kutoka kwao na akaingiwa na hisia ya uoga ndani ya moyo wake. Malaika wakasema, walipoona uoga uliomuingia Ibrāhīm, «Usiogope! Sisi ni Malaika wa Mola wako tumetumwa kwenda kwa watu wa Lūṭ kuwaangamiza.