Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Hud 11:78

11:78
وجاءه قومه يهرعون اليه ومن قبل كانوا يعملون السييات قال يا قوم هاولاء بناتي هن اطهر لكم فاتقوا الله ولا تخزون في ضيفي اليس منكم رجل رشيد ٧٨
وَجَآءَهُۥ قَوْمُهُۥ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِى هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ فِى ضَيْفِىٓ ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌۭ رَّشِيدٌۭ ٧٨
وَجَآءَهُۥ
قَوۡمُهُۥ
يُهۡرَعُونَ
إِلَيۡهِ
وَمِن
قَبۡلُ
كَانُواْ
يَعۡمَلُونَ
ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ
قَالَ
يَٰقَوۡمِ
هَٰٓؤُلَآءِ
بَنَاتِي
هُنَّ
أَطۡهَرُ
لَكُمۡۖ
فَٱتَّقُواْ
ٱللَّهَ
وَلَا
تُخۡزُونِ
فِي
ضَيۡفِيٓۖ
أَلَيۡسَ
مِنكُمۡ
رَجُلٞ
رَّشِيدٞ
٧٨
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watu wa Lūṭ wakamjia kwa haraka kutaka kufanya uchafu, na kabla ya kuja kwao walikuwa wanawendea wanaume kwa njia ya matamanio badala ya wanawake. Lūṭ akasema kuwaambia watu wake, «Hawa ni watoto wangu wa kike, waoeni. Wao niwasafi zaidi kwenu kuliko hayo mnayoyataka.» Aliwaita kuwa ni watoto wake wa kike sababu Nabii wa umma ana daraja ya baba kwao. «Basi muogopeni Mwenyezi Mungu na mjihadhari na mateso Yake, wala msinifedhehi kwa kuwakosea wageni wangu. Kwani hakuna mtu yoyote katika nyinyi aliye mzuri wa kupima mambo apate kuwakataza wanaotaka kufanya machafu akawzuia wao na hayo? Kumdhalilisha mgeni ni jambo la kutukanisha hakuna alifanyalo isipokuwa ni watu wa utwevu.»