Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng'olewa juu ya ardhi. Hauna imara. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mfano wa neno ovu, nalo ni neno la ukafiri, ni kama mti muovu wa chakula na ladha, nao ni mti wa subili, uliong’olewa juu ya ardhi, kwa kuwa mizizi yake iko karibu na uso wa ardhi, hauna mizizi iliyojikita ndani wala hauna tagaa zenye kwenda juu. Hivo ndivyo kafiri alivyo, hana uthabiti wala hana wema na wala hakuna tendo lema lake lolote litakalopaishwa kwa Mwenyezi Mungu.