Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ibrāhīm anamsifu Mola wake na anasema, «Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyeniruzuku, pamoja na uzee wangu, wanangu wawili, Ismā'īl na Isḥāq, baada ya maombi yangu Anitunuku miongoni mwa wema, kwani Mola wangu ni mwenye kusikia maombi ya mwenye kumuomba; na mimemuomba na Hakuyapitisha patupu matarajio yangu.