Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na usidhani, ewe Mtume, kwamba Mwenezi Mungu ni mwenye kughafilika na yale wanayoyafanya madhalimu, ya kukukanusha wewe na Mitume wengine na kuwakera Waumini na maasia mengineyo. Kwa kweli, Anachelewsha kuwatesa mpaka Siku ngumu ambayo macho yao yatakodoka na hayatafumbika kwa kitisho cha yale yanayoyaona. Katika hii pana kumliwaza Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukiye.