Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa kweli, washirikina walimpangia njama Mtume, rehema na amani zimshukie, za kumuua. Na vitimbi vyao vilikuwako kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Yeye Amewazunguka. Na vitimbi vyao vikawarudia wenyewe. Na havikuwa vitimbi vyao ni vyenye kuondoa majabali wala vitu vinginevyo kwa udhaifu wake na unyonge wake. Na wao hawakumdhuru Mwenyezi Mungu, lakini walijidhuru wenyewe.