Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ibrahim 14:5

14:5
ولقد ارسلنا موسى باياتنا ان اخرج قومك من الظلمات الى النور وذكرهم بايام الله ان في ذالك لايات لكل صبار شكور ٥
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَآ أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرْهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍۢ لِّكُلِّ صَبَّارٍۢ شَكُورٍۢ ٥
وَلَقَدۡ
أَرۡسَلۡنَا
مُوسَىٰ
بِـَٔايَٰتِنَآ
أَنۡ
أَخۡرِجۡ
قَوۡمَكَ
مِنَ
ٱلظُّلُمَٰتِ
إِلَى
ٱلنُّورِ
وَذَكِّرۡهُم
بِأَيَّىٰمِ
ٱللَّهِۚ
إِنَّ
فِي
ذَٰلِكَ
لَأٓيَٰتٖ
لِّكُلِّ
صَبَّارٖ
شَكُورٖ
٥
Na tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe watu wako kwenye giza uwapeleke kwenye mwangaza. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa hakika tulimtuma Mūsā kwa Wana wa Isrāīl na tukamsaidia kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake na tukammpa amri awalinganie wao kwenye Imani, ili awatoe wao kutoka kwenye upotevu awatie kwenye uongofu na awakumbushe neema za Mwenyezi Mungu na mateso Yake katika wakati wake. Katika kukumbusha huku mambo hayo kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, kuyaepuka yaliyoharamishwa na Yeye na kuyakubali maandiko Yake, mwenye kushukuru sana, mwenye kusimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na anayemshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake. Aina mbili hizi za watu zimetajwa mahsusi, kwa kuwa wao ndio wanaozingatia hizo dalili na hawaghafiliki nazo.