Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Luqman 31:30

31:30
ذالك بان الله هو الحق وان ما يدعون من دونه الباطل وان الله هو العلي الكبير ٣٠
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلْبَـٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ ٣٠
ذَٰلِكَ
بِأَنَّ
ٱللَّهَ
هُوَ
ٱلۡحَقُّ
وَأَنَّ
مَا
يَدۡعُونَ
مِن
دُونِهِ
ٱلۡبَٰطِلُ
وَأَنَّ
ٱللَّهَ
هُوَ
ٱلۡعَلِيُّ
ٱلۡكَبِيرُ
٣٠
Hivi ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanacho kiomba ni cha uwongo. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu na ndiye Mkubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yote hayo ni miongoni mwa ukubwa wa uweza Wake. Mpate kujua na mkubali kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye wa kweli katika dhati Yake na sifa Zake na matendo Yake, na kuwa vile wanavyoviomba visivyokuwa Yeye ndio vya urongo, na kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyetukuka, kwa dhati Yake, uweza Wake na kutendesha nguvu Kwake, Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, Aliye Mkubwa juu ya kila kitu, na kila kisichokuwa Yeye kinanyenyekea Kwake, Yeye Peke Yake Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, na si mwingine.