Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
019

Maryam 19:5 واني خفت الموالي من ورايي وكانت امراتي عاقرا فهب لي من لدنك وليا ٥

19:5
وَإِنِّي
خِفۡتُ
ٱلۡمَوَٰلِيَ
مِن
وَرَآءِي
وَكَانَتِ
ٱمۡرَأَتِي
عَاقِرٗا
فَهَبۡ
لِي
مِن
لَّدُنكَ
وَلِيّٗا
٥
Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

«Na mimi ninaogopa kwamba jamaa zangu wa karibu na wenye kusimama na mimi wasije, baada ya kufa kwangu, wakaacha kuisimamia Dini yako vile inavyotakikana isimamiwe na wakaacha kuwalingania waja wako kuwaleta kwako, na mke wangu ni tasa hazai, basi nitunukie kutoka kwako mtoto awe ni mrithi na msaidi…
«Na mimi ninaogopa kwamba jamaa zangu wa karibu na wenye kusimama na mimi wasije, baada ya kufa kwangu, wakaacha kuisimamia Dini yako vile inavyotakik…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 19, Ukurasa 305, Juzuu 16

1. Kaf Ha Ya A'yn S'ad. 2. Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya. 3. Alipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri. 4. Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe. 5. Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako. 6. Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha. 7. (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake. 8. Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimesha fikia ukongwe katika uzee? 9. Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu. 10. Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima. 11. Basi akawatokea watu wake kutoka mihirabuni. Akawaashiria: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni. 12. Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto. 13. Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mcha mungu. 14. Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari muasi 15. Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia