Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Muhammad 47:30

47:30
ولو نشاء لاريناكهم فلعرفتهم بسيماهم ولتعرفنهم في لحن القول والله يعلم اعمالكم ٣٠
وَلَوْ نَشَآءُ لَأَرَيْنَـٰكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَـٰهُمْ ۚ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِى لَحْنِ ٱلْقَوْلِ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ أَعْمَـٰلَكُمْ ٣٠
وَلَوۡ
نَشَآءُ
لَأَرَيۡنَٰكَهُمۡ
فَلَعَرَفۡتَهُم
بِسِيمَٰهُمۡۚ
وَلَتَعۡرِفَنَّهُمۡ
فِي
لَحۡنِ
ٱلۡقَوۡلِۚ
وَٱللَّهُ
يَعۡلَمُ
أَعۡمَٰلَكُمۡ
٣٠
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na lau tungalitaka, ewe Nabii, tungalikuonesha hao watu wenyewe, ukawatambua kwa alama zilizo wazi kwao. Na kwa hakika utawajua kutokana na maneno yao yaliyodhihirika yenye kuonyesha malengo yao. Na kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hakuna chochote kinachofichamana cha matendo ya wanaomtii wala matendo ya wanaomuasi, na Atamlipa kila mmoja kwa anachostahili.