Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Muhammad 47:31

47:31
ولنبلونكم حتى نعلم المجاهدين منكم والصابرين ونبلو اخباركم ٣١
وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ ٱلْمُجَـٰهِدِينَ مِنكُمْ وَٱلصَّـٰبِرِينَ وَنَبْلُوَا۟ أَخْبَارَكُمْ ٣١
وَلَنَبۡلُوَنَّكُمۡ
حَتَّىٰ
نَعۡلَمَ
ٱلۡمُجَٰهِدِينَ
مِنكُمۡ
وَٱلصَّٰبِرِينَ
وَنَبۡلُوَاْ
أَخۡبَارَكُمۡ
٣١
Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapignao Jihadi katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tutawatahini nyinyi, tena tutawatahini, enyi Waumini, kwa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu na kupigana nao jihadi mpaka yajitokeze yale Aliyoyajua Mwenyezi Mungu tangu kale, ili tuwatenge watu wa jihadi kati yenu na uvumilivu wa kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu na tuyatahini maneno yenu na matendo yenu, na hapo adhihirike mkweli miongoni mwenu kutokana na mrongo.