Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Muhammad 47:32

47:32
ان الذين كفروا وصدوا عن سبيل الله وشاقوا الرسول من بعد ما تبين لهم الهدى لن يضروا الله شييا وسيحبط اعمالهم ٣٢
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّوا۟ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا۟ ٱللَّهَ شَيْـًۭٔا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَـٰلَهُمْ ٣٢
إِنَّ
ٱلَّذِينَ
كَفَرُواْ
وَصَدُّواْ
عَن
سَبِيلِ
ٱللَّهِ
وَشَآقُّواْ
ٱلرَّسُولَ
مِنۢ
بَعۡدِ
مَا
تَبَيَّنَ
لَهُمُ
ٱلۡهُدَىٰ
لَن
يَضُرُّواْ
ٱللَّهَ
شَيۡـٔٗا
وَسَيُحۡبِطُ
أَعۡمَٰلَهُمۡ
٣٢
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika ya wale waliokataa kuwa Menyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, wakawazuia watu na Dini Yake, wakaenda kinyume na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakampiga vita baada ya wao kujiwa na hoja na alama za kuwa yeye ni Nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawataidhuru Dini ya Mwenyezi Mungu kitu chochote na Atayatangua malipo ya matendo yao waliyoyafanya duniani, kwa kuwa wao hawakutaka kwa matendo hayo radhi za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.