Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa hakika tuliumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe kwa muda wa Siku sita, na hatukupata tabu yoyote wala shida. Katika uweza huu mkubwa kuna dalili ya nguvu zaidi ya kuwa Yeye, Aliyetakasika, Ana uweza wa kuhuisha wafu.