Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yale wanayoyasema wakanushaji, kwani Mwenyezi Mungu Yuko chonjo nao. Na swali, kwa ajili ya Mola wako kwa kumshukuru, Swala ya Alfajiri, kabla ya jua kuchomoza, na Swala ya Alasiri kabla ya jua kuchwa,